Mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania Millen Hapinnes Magese (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es S...
Mwanamitindo
wa kimataifa wa Tanzania Millen Hapinnes Magese (kushoto) akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni MMG Africa
Ms. Lucy Ngongoseke.
Na.MO BLOG TEAM
Mwanamitindo
wa kimataifa wa Tanzania Millen Hapinnes Magese anakusudia kuitangaza
nchi hii kimataifa kupitia fani ya mitindo Tanzania International
Fashion Expose (TIFEX) kwa kuendesha zoezi la kutafuta wanamitindo
wawili vijana watakaoshiriki kwa mara ya kwanza katika maonyesho ya Wiki
ya Mavazi ya Afrika Kusini (South Africa Fashion Week).
Zoezi
la kuwatafuta wanamitindo hao kwa vijana wa kike na kiume litaendeshwa
chini ya kampuni yake ya Millen Magese Group Company Limited
yanayotarajiwa kufanyika tarehe 1 April mwaka huu.
Magese
amesema wanamitindo vijana wanaotaka kupata nafasi ya kuiwakilisha
Tanzania wafike siku ya Jumapili tarehe 25 mwezi huu kwa ajili ya mchujo
huo kuanzia saa 8 mchana utakaofanyika katika Hoteli ya Serena.
Amesema kuwa hiyo ni fursa peke kwa wanamitindo kuweza kujitangaza wenyewe kimataifa na kufuata nyayo zake.