mwanzo Mchuchumio:Viatu hatari kwa afya ya miguu ya wanawake

  Wanawake wenye maumbo ya kati, ambao si wanene wala wembamba wamekuwa wakipendelea viatu virefu.PICHA|MAKTABA  ...

 
Wanawake wenye maumbo ya kati, ambao si wanene wala wembamba wamekuwa wakipendelea viatu virefu.PICHA|MAKTABA 
Na  Ibrahim Bakari, Mwananchi

Posted  Ijumaa,Decemba27  2013  saa 16:44 PM
Kwa ufupi
Wengi, hasa wasichana wa kisasa. huamini kuwa viatu hivi vinawafaa, kumbe vina madhara kwao


‘Mchuchumio’ ama viatu vyenye visigino virefu, ni mojawapo ya vitu vinavyopendwa na baadhi ya wanawake mbalimbali, si katika Tanzania bali dunia nzima.
Wataalamu wanaeleza kuwa viatu hivi huharibu pingili za uti wa mgongo na huvunjavunja mifupa ya visigino.
Wanawake wenye maumbo ya kati, ambao si wanene wala wembamba wamekuwa wakipendelea viatu virefu.
Kwa kiasi kikubwa wasichana wafupi, wamekuwa wakipendelea kuvaa viatu virefu ili angalau na wao waonekane warefu.
Ashura Mgweno, mfanyakazi wa Kampuni ya Usafi jijini Dar es Salaam, anasema: “Nimetumia viatu kwa muda mrefu, lakini sasa sitaki kusikia viatu virefu. Mimi ni mfupi, nilikuwa navaa sana, lakini sasa sitaki hata kuviona jinsi vilivyonitesa,” anasema.
Anasema kuwa viatu virefu muda wake ni miaka mitatu, inaharibu visigino na misuli ya miguu na kutengeneza vigimbi ambavyo baadaye husababisha maumivu makali.
Akizungumzia hili, Ruth Erasto ambaye anafanya kazi katika ofisi moja jijini Dar es Salaam, anasema aliacha kuvaa ‘mchuchumio’ kwa maagizo ya daktari.
“Niligawa viatu vyangu vyote virefu baada ya kupatwa na maumivu ya mgongo. Viatu virefu havilinganishi mwili wakati wa kutembea na niliagizwa na daktari kuachana na viatu virefu...hiyo ilitokana na mimi kuanza kupatwa na matatizo ya mgongo,” anasema.
Anasema kuwa alipatwa na matatizo hayo bila kufahamu, lakini baada ya kuchunguzwa, ndipo ikabainika kupatwa na matatizo hayo.
Mwanamama mwingine aliyepatwa na matatizo hayo, Victoria, anasema kuwa inamlazimu kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kila mara kwa ajili ya kuangaliwa maendeleo ya mgongo baada ya kuvaa viatu virefu kwa muda mrefu na kumletea athari hizo.
Victoria ambaye ni mfupi na mnene kiasi kwa umbile, anasema kuwa pamoja na kupenda kuvaa viatu hivyo, hataki kusikia habari zake.
“Nakuambia sina hamu na viatu hivi, acha kabisa, nimekoma...nimekwenda Muhimbili hadi nimechoka, maumivu kuanzia kiuno hadi mgongo,” anasema.

Name

Fasheni Mavazi Miss Tz Mitindo Modo Urembo Viatu
false
ltr
item
PAMBAIKA TZ: mwanzo Mchuchumio:Viatu hatari kwa afya ya miguu ya wanawake
mwanzo Mchuchumio:Viatu hatari kwa afya ya miguu ya wanawake
http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/2126758/highRes/653120/-/maxw/600/-/n27m1/-/mchuchumo.jpg
PAMBAIKA TZ
https://pambaikatz.blogspot.com/2014/11/mwanzo-mchuchumioviatu-hatari-kwa-afya.html
https://pambaikatz.blogspot.com/
http://pambaikatz.blogspot.com/
http://pambaikatz.blogspot.com/2014/11/mwanzo-mchuchumioviatu-hatari-kwa-afya.html
true
5133514619242769278
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy